Kwa mujibu shirika la habari la IRNA, Masoud Pezeshkian, Rais wa Iran, Alhamisi usiku katika mazungumzo ya simu na Mahdi al-Mashat, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, alitoa pongezi kwa mnasaba wa Sikukuu ya Idd El-Fitr na kusisitiza kuwa: “Waislamu wanapaswa kuwa na mshikamano na umoja ili maadui wasiweze kuyadhulumu mataifa ya Kiislamu.”
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, naye pia alimpongeza Rais wa Iran, wananchi wa Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mnasaba wa Sikukuu ya Idd El-Fitr, na kusema: “Misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono umoja wa Kiislamu ni ya kujivunia kweli.”
Masoud Pezeshkian, Rais wa Iran, katika siku za hivi karibuni amekuwa akizungumza na viongozi wa nchi jirani na za Kiislamu, ambapo katika kipindi hiki cha vitisho na mashinikizo kutoka kwa maadui wenye dhulma na kiburi, amekuwa akijitahidi kuleta ari mpya katika uhusiano wa kidiplomasia wa kikanda, pamoja na kuchukua hatua za kuimarisha ushirikiano na mataifa rafiki, jirani na washirika.
Katika mazungumzo ya simu na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia Mohammad bin Salman, Rais wa Iran amesisitiza kwa kusema: "Nina imani kwamba kama nchi za Kiislamu zifanya kazi kwa pamoja, zinaweza kuleta usalama na ustawi bora katika eneo hili."
Aidha katika mazungumzo na Rais Kais Saied wa Tunisia, Rais wa Iran amesema umoja na mshikamano miongoni mwa mataifa ya Kiislamu unaweza kuwa chachu ya kukomeshwa jinai za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
342/
Your Comment